Jumanne. 30 Aprili. 2024

Mt. Simoni na Yuda

Simoni na Yuda

Habari zijulikanazo juu ya mitume hao ni chache. Walichaguliwa na Yesu kutoka katika kundi la wafuasi waKe ili wawe mitume. 'Mtume' ni mtu anayetumwa.

Husemwa kwamba walishirikiana kufanya kazi kama wamisionari katika nchi ya Uajemi, na hukohuko waliuawa kwa ajili ya Bwana Yesu. Kwa sababu hiyo, wanaiadhimisha sikukuu yao pamoja katika siku hiyo moja.

Mtume Simoni ameitwa 'Zeloti' yaani 'mwenye bidii' kwa sababu alifanya bidii kutangaza kokote dini ya Yesu Kristu. Mtume Yuda anaitwa 'Tadayo' (Mt. 10:3) maana yake 'Hodari' ili kumtofautisha na Yuda Iskarioti, msaliti. Alikuwa ndugu wa Mtume Yakobo mdogo (taz. 3 Mei), tunavyosoma katika Injili, na anavyosema mwenyewe katika Barua yake yenye kujulikana kama "Barua ya Yuda". Barua hii aliandika kwa makanisa yaliyo karibu na Nchi Takatifu kama alivyofanya nduguye katika "Barua ya Yakobo".

Mt. Yuda Tadayo huheshimiwa pia kama 'Kimbilio katika hali zote zilizo mbaya sana'.

Maoni


Ingia utoe maoni