Jumanne. 30 Aprili. 2024

Mt. Kosmasi na Damiano

Kosmasi na Damiano

COSMAS NA DAMIANO MASHAHIDI
Watakatifu mashahidi wafiadini Cosmas na Damiano tunaowakumbuka leo walikuwa ndugu mapacha waliozaliwa huko Arabia miaka ya mwanzo ya Ukristo. walisoma na kufudhu vizuri katika tiba na sayansi ya madawa. Tangu utoto wao Cosmas na Damiano walijawa na moyo wa upendo na kuwahudumia watu.

kama wakristo, walitumia taaluma yao kuwahudumia wagonjwa. kama matatibu walipata fursa za kuingia katika nyumba za wapagani kutoa huduma. Walipendwa sana na watu wote kwani kamwe hawakuchukua fedha kwa huduma walizozitoa, hivyo watu waliwaita “Watakatifu bila fedha”

Muujiza wa Cosmas na Damiano. Inasemekana walimponya mtu aliyepata shida ya mguu. kwa msaada wa Mungu walimbadilishia mkuu mtu mweupe aliyekuwa mgonjwa kwa kumwekea mguu wa mtu mweusi wa Ethiopia aliyekuwa amekufa karibuni.

wakati wa madhurumu ya Diokletiani, Watakatifu Cosmas na Damiano waliteswa vikali na hatimaye kuuawa kwa sababu ya imani yao. Watakatifu Cosmas na Damiano ni wasimamizi na waombezi wa Wafamasia.

Maoni


Ingia utoe maoni