Jumamosi. 23 Novemba. 2024

Mt. Seraphin wa Monte

Seraphin wa Monte

Mt. Seraphin alizaliwa huko Italia mwaka 1540 katika familia ya kimaskini ya Jerome De Nicola na Theodora. Wazazi hawa walimlea katika maadili bora akiwa na jina Felix. kwasababu ya hali ya familia yake, Felix alifanya kazi ya kuchunga mifugo. akiwa na miaka 16, alijiunga na wakapuchin na kupewa jina Seraphin alipoweka nadhiri. Akiwa utawani, Seraphin alidhihirisha moyo wa ibada na kila siku alitumia saa 3 akisali mbele ya Ekaristi takatifu. Alikuwa mpole, nnyenyekevu na mkarimu kiasi kwamba hata wale ombaomba waliofika katika monasteri kupata chochote, walimtafuta yeye. Aliipenda sana Ekaristi na kuwapenda na kuwaheshimu mapadre. Kwa mfano wa Mt. Francis wa Asis, alipenda kuibusu mikono ya padre, kwani kwake alimpokea Kristo aliyenguvu na asili ya kila lililojema. Pia alijiweka chini ya ulinzi na usimamizi wa Mama Maria, akaamini “per Mariam ad Jesum, kwa njia ya Maria tunamwendea Yesu”. Mt. Seraphin alifariki 12/1604 na kutajwa Mtakatifu na Papa Clement XIII tarehe 16/7/1767

Maoni


Ingia utoe maoni