Jumatano. 04 Desemba. 2024

Mt. Robert Bellarmino

Robert Bellarmino

Mtakatifu Robert Bellarmino alizaliwa huko Montepulciano, Italia ,mwaka 1542, mwezi oktoba tarehe 4.

Alikuwa mtoto wa 3 katika familia ya watoto 10.

Baba yake aliitwa Vincenzo Bellarmino na mama yake aliitwa Cinzia Cervini.

Alijiunga na Wa Jesuit mwaka 1560, katika nyumba yao huko Mondovi,Piedmont.

Huko alijifunza pia kigiriki. Kutokea hapo alipelekwa katika chuo kikuu cha Padua. Hapo alisoma teolojia kati ya mwaka 1567 na 1568.Mwaka 1569 alikwenda kumalizia masomo yake katika chuo kikuu cha Lauven huko Flanders ( Ubelgiji ).

Akapata daraja la upadri na pia akawa profesa. Akawa Mjesuit wa kwanza kufundisha katika chuo kikuu.

Miaka saba baadae aliondoka Lauven kutokana na matatizo ya afya yake.Mwaka 1576 alirudi Italia. Akapewa kazi ya kufundisha katika chuo kilichoitwa New Roman College (Pontifical Gregorian University) na papa Gregory XIII.

Mpaka mwaka 1589 Mt Bellarmino alikuwa akifundisha kama profesa wa teolojia. Mwaka 1592 Pope Clement VIII alimchagua kuwa mkuu wa chuo, akawa askofu, akiwafundisha maaskofu pia.

Mwaka 1599 aliteuliwa kuwa Kardinali .Mwaka 1602 aliteuliwa kuwa Askofu mkuu wa Capua. Hapo aliandika vitabu vyenye mafundisho na machapisho mengi.

Katika uzee,akaamishiwa Montepulciano, alikozaliwa ambako kwa miaka minne alikuwa Askofu .Akaamua kupumzika na kurudi katika chuo cha Wa Jesuit cha mt Andrew huko Roma.

Mtakatifu Robert Bellarmino alikufa tarehe 17 Oktoba 1621 huko Roma.

Alitangazwa mwenye heri mwaka 1923 ,13 Mei na Papa Pius XI na akatangazwa Mtakatifu mwaka 1930 Juni 29.

Maoni

Robert Boaz

asante sana kwa kutusogezea habari njema, hii ni historia ya maisha ya Mtakatifu somo wangu, niliitafuta kitambo bila mafanikio, amani iwe nawe

Ingia utoe maoni