Ijumaa. 19 Aprili. 2024

Mt. Januarius (Januari)

Januarius (Januari)

Mtakatifu Januarius (Januari) Askofu na Shahidi

Mtakatifu Januarius alizaliwa katika mji wa Benevento huko Italia, katika familia ya kitajiri. Akiwa na miaka 15 tu alipata daraja la upadri, na akafanya kazi katika parokia ya Benevento. Muda huo kulikuwa na wapagani wengi katika mji huo.

Akiwa na miaka 20, alipata daraja la Uaskofu na kuwa Askofu wa Naples. Katika muda huo, mfalme Diocletian, ambaye alikuwa mpinga Kristo alitawala. Mfalme huyo aliendesha madhulumu kwa wakristo, akiwakamata, kuwafunga na kuwauwa.

Mtakatifu Januarius, aliwaficha baadhi ya wakristo, na kuwaepusha na mateso. Lakini rafiki yake alikamatwa. Huyo alikuwa Mtakatifu Sissou.

Mtakatifu Januarius, aliamua kwenda kumtembelea gerezani, naye pia akakamatwa. Mfalme akaamuru wauwawe kwa kutupwa kati ya wanyama wakali, katika uwanja huko Pozzuoli.

Lakini kwa kuogopa fujo kutoka kwa watu wa mji ule, hukumu ikabadilishwa. Ikatakiwa auwawe kwa kukatwa kichwa.
Mtakatifu Januarius, aliuwawa kwa kukatwa kichwa, katika kreta ya Solfatara, karibu na mji wa Pozzuoli. Ilikuwa mwaka 305.

Maoni


Ingia utoe maoni