Jumatano. 04 Desemba. 2024

Mt. Katarina wa Siena

Katarina wa Siena

Mtakatifu Katarina alizaliwa mwaka 1347,March 25 huko Siena Italia.Alikuwa mmoja kati ya watoto 25 waliozaliwa na mama yake.Kati ya hao nusu walikufa wakiwa wachanga.
Akiwa na miaka 16,dada yake aliyeitwa Bonaventura alifariki.Wazazi wake walimtaka aolewe na shemeji yake,lakini alikataa.Aliamua kufunga,akakata nywele,ili abadilishe muonekano wake.Baadae wazazi wake waliamua kuacha dhamira yao,wakamuache afuate uelekeo aupendao.Akajiunga na utawa wa 3 wa Mt Dominic,ambao ulimpa ruhusa ya kukaa nyumbani kwao,akifanya shughuli za utawa ule.Watawa wenzie wakamfundisha kusoma na kuandika.Kutokana na moyo wa huruma aliokuwa nao,alianza tabia ya kugawia vitu wahitaji.Aligawa chakula,nguo nakadhalika.Hakuomba ruhusa ya mtu katika kufanya hayo,jambo lililomletea kutokuelewana nyakati zingine.Katarina alikuwa na maono ya kusaidia watu ,hivyo aliamua kuingia mitaani kwa watu maskini,wagonjwa na kusaidia kila alichoweza.Watu wakavutiwa na hilo na wengine wakaamua kumfuata na kufanya nae kazi mbalimbali.Alianza kusafiri kwenda sehemu mbalimbali akiwahimiza watu kuungama na kumpenda Mungu kwa ukweli.Aliwaomba wakristu wawe na utii kwa Papa.Alihimiza pia kuanzishwa kwa vita vya msalaba kukomboa nchi takatifu.Katika tukio moja alimtembelea mfungwa aliyehukumiwa kifo,akamfanya mtu yule atambue uwepo wa Mungu.Alikubali na hata adhabu yake ilipotimizwa,alikufa katika amani.Aliendelea kuhimiza amani na upendo kwa watu wote,akaanzisha kituo cha wanawake watawa mwaka 1377 nje ya Siena,akaandika barua 400,zikiwemo sala,.Mwaka 1380,akiwa na miaka 33 tu,aliugua sana kutokana na kufunga sana.Akaugua kwa mud a,hadi mwezi April 29 ambapo alikufa.

Maoni


Ingia utoe maoni