Jumatano. 04 Desemba. 2024

Mt. Petro wa Verona

Petro wa Verona

Mt Petro,alizaliwa Verona mwaka 1205.Wazazi wake walikuwa wapagani.Lakini Petro alisoma katika shule za wakatoliki na baadae alijiunga na chuo kikuu cha Bologna.Akiwa Bologna,Petro alikubaliwa katika shirika la wadominican na mt Dominic Mwenyewe.Akaondokea kuwa mhubiri mzuri,na namna yake ya kufanya ibada ikawavutia mno watu wa jimbo la Lombardy.Mwaka 1234 aliteuliwa na Papa Gregory lX kuongoza mpango wa kuhubiri katika Italia ya kaskazini,ambako kulikuwa na wapagani wengi.Mahubiri yaliwavuta wengi,na hata hivyo alipata maadui pia.Mwaka 1252,akiwa anatoka Como kwenda Milan aliuwawa akiwa na miaka 46.Mwaka uliofuata alitangazwa mtakatifu na Papa Innocent IV.

Maoni


Ingia utoe maoni