Jumatano. 04 Desemba. 2024

Mt. Magdalena wa Cannosa

Magdalena wa Cannosa

Mtakatifu Magdalena alizaliwa Verona Italia, tarehe 1 Marchi 1774,akiwa mtoto wa pili,kl katika familia ya kiungwana. Baba yake alikufa wakati akiwa na miaka 5.

Akiwa na miaka 17, aliamua kumtumikia Mungu. Alijiunga na shirika la Wa Carmel na kutoka Roho Mtakatifu akimtaka kufuata njia mpya. Hapo ndipo alipoanza kazi ya kusaidia watu walioumia katika vita iliyotokana na mapinduzi ya Ufaransa. Akawa pia akihudumia wagonjwa na pia, akaanza kuwaangalia na kuwasaidia wasichana wanaoishi katika mazingira magumu, na waliotelekezwa.

Mwaka 1808, Mtakatifu Magdalena alihama katika nyumba ya familia yao, akifuatana na wanawake wachache, akaenda kuanzisha makazi katika wilaya ya San Zeno. Hapo akaanzisha kundi dogo, aliloliita Daughters of Charity.

Tarehe 23 December 1828, Daughters of Charity ilikubaliwa na Papa Leo XII. Kutokea hapo, walimudu kufungua nyumba mbalimbali, na kuendelea kusaidia na kuelimisha jamii, katika sehemu mbalimbali.

Mtakatifu Magdalena alikufa mwaka 1835 April 10, huko Verona kwa amani. Alitangazwa mwenye heri mwaka 1941 December 8 na Papa Pius XII, na kutangazwa mtakatifu tarehe 2 October 1988 na Papa John Paul II tarehe 2 October 1988

Maoni


Ingia utoe maoni