Jumatano. 04 Desemba. 2024

Mt. Nikola wa Tolentino

Nikola wa Tolentino

Mtakatifu Nikola wa Tolentino, Padri
Mtakatifu Nikola alizaliwa mwaka 1246, huko Italia.Aliingia utawa akiwa na miaka 18, na miaka 7 baadaye akapata daraja la Upadri.

Mtakatifu Nikola alipata umaarufu mkubwa kwa namna alivyoweza kuhubiri.
Mwaka 1274 alitumwa kwenda kufanya kazi katika mji wa Tolentino, karibu na alipozaliwa.Nyakati hizo kulikuwa na mgawanyiko kati ya wakazi wa mji huo.

Kuna kundi lililomkubali na kumfuata Papa, na kundi lililomkubali na kumfuata mtawala wa dola ya Kirumi. Lakini Mtakatifu Nikola, alifanya kazi katika makundi yote, akihudumia maskini na wahitaji.Alikuwa pia na nguvu ya uponyaji kwa sala na imani.

Mtakatifu Nikola alikufa mwaka1305 September 10,huko Tolentino.Akatangazwa Mtakatifu mwaka 1446 June 5 na Papa Eugene IV.

Maoni


Ingia utoe maoni