Laurenti Yustiniani
Mtakatifu Laurenti, alizaliwa mwaka 331 Julai 1 huko Venice, Italia. Baada ya masomo yake, mwaka 1404, alipata daraja la Ushemasi.
Akajiunga na monasteri ya mtakatifu George,huko Alga.Mwaka 1406, akapata daraja la Upadri.
Akafanya kazi ya Mungu kwa bidii, akisali na kufanya majitoleo mbalimbali.Mwaka 1433, alichaguliwa na Papa Eugenius IV, kuwa Askofu wa Castello.
Mwaka 1451 Baba Mtakatifu aliunganisha jimbo la Castello na jimbo la Grado kuwa jimbo la Venice. Mta akachaguliwa kuwa Askofu wa kwanza wa Venice.
Mtakatifu Laurenti alifanya kazi kwa bidii, akifuata haki na kweli.Akapendwa na watu wengi, akasaidia katika mambo ya utawala katika serikali iliyokuwepo.
Mtakatifu Laurenti alikufa mwaka 1456 Januari 8.
Alitangazwa mwenyeheri mwaka 1524 na Papa Clement VII .Akatangazwa Mtakatifu mwaka 1690 October 16 na Papa Alexander VIII.
Maoni
Ingia utoe maoni