Antoni Maria Klareti
Mtakatifu Antoni, alizaliwa tarehe 23 December 1807, huko Sallent, Barcelona Hispania.Alikuwa mtoto wa 5 kati ya watoto 11 wa Juan na Josefa Claret. Baba yake alikuwa akitengeneza nguo.
Mtakatifu Antoni, alipata elimu ya awali katika shule iliyokuwa hapo hapo katika mji aliozaliwa. Akiwa na miaka 18, baba yake alimpeleka Barcelona, kujifunza kuhusu biashara ya nguo.Na pia alipata muda wa kusoma, akajifunza Kilatini na kifaransa.
Wito wa kumtumikia Mungu ulipomfikia, aliondoka Barcelona, na mwaka 1829 akajiunga na seminari ya jimbo alipotoka. Mwaka 1835 June 13, alipata daraja la upadri. Akafanya kazi katika parokia ya hapo kwao, huku akiendelea kusoma teolojia , mpaka mwaka 1839.
Akaenda Roma, ambako alijiunga na shirika la Wa Jesuit, lakini alilazimika kuondoka kutokana na tatizo la afya yake.Akarudi tena Hispania.
Akasaidia katika miji ya Viladrau na Girona, ambayo watu wengi walikuwa wameathirika na vita. Akatumwa na wakuu wake kwenda kuhubiri katika Catalonia, ambako nako kulikuwa na maumivu ya vita , iliyotokana na uvamizi wa Wafaransa.
Huko Catalonia, alitembea kwa miguu, jimbo lote, akihubiri na kurejesha imani ya wakristo wengi waliopotea. Maisha yake yakawa hatarini , ikamlazimu kwenda katika kisiwa cha Canary mwaka 1848, kuepuka vuguvugu za wapinga Kristo.
Mtakatifu Antoni, alirudi Hispania na kuanzisha shirika (Congregation of the Missionary Sons of the Immaculate Heart of Mary ) la wa Claretians tarehe 16 Julai 1849.Akaanzisha pia maktaba kubwa ya dini mjini Barcelona ambayo aliita "Libreria Religiosa" (sasa Libreria Claret).Mwaka 1865 December 22 alipata ruhusa rasmi kwa ajiri ya shirika aliloanzisha,toka kwa Papa Pius IX .
Mwaka 1849 alichaguliwa na Papa, kuwa Askofu wa Santiago huko Cuba.Akasimikwa rasmi mwaka 1850.
Katika utumishi wake huko Cuba, ndani ya miaka 2, alirejesha nidhamu na upendo, zikafungwa ndoa zaidi ya 9,000.Akajenga mahospitali na mashule.
Akaanzisha shule za ufundi kwa wasio na vipato , vyama vya kukopeshana , na akatunga vitabu kufundisha kilimo.
Akaanzisha shirika la watawa mwaka 1855, akisaidiana na Antonia Paris, ambalo ndilo lililokuwa la kwanza kwa wanawake katika Cuba. Akaanzisha utaratibu wa kutembelea wafungwa na wagonjwa hospitalini.
Kutokana na yote hayo, alipata pia maadui wengi na wauaji walijaribu kumuua, lakini walimjeruhi tu.Mwaka 1857, aliitwa na malkia Isabella II, kurudi
Hispania.
Akaruhusiwa kurudi Hispania na kupewa jimbo la Trajanopolis. Hapo, alianza kusaidia katika elimu, akijenga maktaba, maabara, makumbusho ya historia, vyuo na shule za muziki.
Mwaka 1868, kulitokea mapinduzi katika Hispania , na ikabidi malkia na familia yake wakaishi uhamishoni huko Ufaransa.Ikabidi na Askofu Anthony naye akaishi huko Ufaransa, kabla ya kwenda Roma, na baadaye kurudi tena Hispania
Mwaka 1869, alirudi tena Roma, kutayarisha mkutano mkuu wa Vatican .Lakini alipata maradhi yaliyompelekea kwenda katika nyumba ya watawa ya Fontfroide, Narbonne, Ufaransa, ambapo alikufa tarehe 24 October 1870.
Alitangazwa mwenye heri mwaka 1934 February 24 na Papa Pius XI na akatangazwa mtakatifu mwaka 1950 May 7 na Papa Pius XII.
Mtakatifu Antoni Maria Claret alitangazwa na kualiandika vitabu 144.
Maoni
Ingia utoe maoni