Jumamosi. 04 Mei. 2024

Mt. Bruno

Bruno

Mtakatifu Bruno alizaliwa mwaka1030, huko Cologne, Ujerumani. Alipomaliza masomo yake, alipata daraja la Upadri mwaka 1055.
Mwaka 1056, Askofu Gervais alimuita kwenda mji wa Reims. Katika kipindi cha mwaka mmoja, aliweza kusimamia elimu katika jimbo lote, mpaka mwaka 1075. Watu wengine mashuhuri walisoma chini ya uangalizi wake, akiwemo Papa Urban II.

Mwaka 1075 alichaguliwa kuwa katibu wa jimbo.Baadae alikataa uteuzi wa kuwa Askofu, na yeye na wenzake wachache,waliondoka mjini na kwenda katika jimbo la Langres, karibu na Seche. Huko nako aliondoka, akiambatana na wenzake na kwenda kwa Askofu wa Grenoble. Askofu huyo aliwapa sehemu ya Chartreuse, karibu na milima ya Alps.

Hapo walijenga makazi yao,na waliishi hapo kimaskini, wakisoma, wakisali na kuomba. Mwaka 1090, baada ya Urban II kuwa Papa, alimuita Mtakatifu Bruno kwenda Roma, kuwa mshauri wake.

Mwaka 1091 Mtakatifu Bruno aliomba kukaa katika jimbo la Squillace, katika msitu mdogo. Huko walijenga kanisa dogo na makazi yao.

Mtakatifu Bruno alikufa mwaka 1101 October 6 huko Serra San Bruno, Italia.
Akatangazwa mwenyeheri mwaka 1514 na Papa Leo X na akatangazwa Mtakatifu tarehe 17 Februari 1623 na Papa Gregory XV.

Maoni


Ingia utoe maoni