Daniel Comboni
Alizaliwa huko Italia Machi 15, 1831. Mapema kabisa aliondoka Italia na kuja África ya Kati kutangaza Injili Takatifu. Alijenga misioni nyingi huko.
Aliwekwa kuwa Askofu wa Khartoum mwaka 1877. Alianzisha Shirika la Misionari wa Comboni (The Comboni Missionaries ) na shirika lake linafanyakazi za kitume katika mabara yote duniani katika nchi zaidi ya 40.
Barani Afrika shirika linafanyakazi katika nchi 15 zikiwemo nchi jirani zetu kama Kenya, Uganda, Malawi, Msumbiji, Kongo lakini bahati mbaya Tanzania bado hatuna huduma za shirika hili.
Mtakatifu Daniel Comboni alifariki huko Khartoum Sudani mnamo Oktoba 10, 1881.
Baba Mtakatifu Yohane Paulo II alimtangaza mtkatifu 2003, Oktoba 5 katika Viwanja vya Mtakatifu Petro huko Vatican.
Maoni
Ingia utoe maoni