Malaika Walinzi Wetu
Mungu, kwa wema wake, ametupa sisi sote malaika mmoja wa kutulinda tangu siku ya kuzaliwa kwetu mpaka saa ya kufa kwetu. Watu wote, watakatifu kwa wakosefu, kila mmoja ana malaika wake mlinzi. Malaika mlinzi wetu hutuepusha na hatari zote, hutunza roho zetu, hutukinga katika vishawishi vya shetani na hutushauri rohoni mwetu tuwe na mawazo mema. Kwa maombezi yake, hutupatia nguvu; tukikosa hutuongozatutubu dhambi zetu; hutuombea na kumtolea Mungu sala na matendo yetu mema. Katika saa ya kufa humtuliza mgonjwa katika masumbuko yake, humfukuza shetani anayetaka kutupoteza. Roho yetu ikisha kututoka, huileta burazani kwu Mungu. Hufurahi kama mtoto aliyemsinumia, atakwenda kukaa mbinguni milele. Mtakutifu Bernardo, abati wa Klervo (tazama 20 Agosti), aliscma kwamba siku moja alipokuwa akisali pamoja na wenzake kanisani, akamwona malaika aliyeandika, kwa herufi mbalimbali, sala zao kadiri walivyosali vizuri au vibaya. Sala za mmoja wao aliziandika kwa herufi ya dhahabu, za mwingine kwa herufi za fedha, na za mwisho kwa wino tu. Sala za wamonaki wengine, waliotawanya mawazo yao kwa makusudi, hazikuandikwa hata.
Ijapo hatumwoni Malaika Mlinzi wetu, tufahamu yupo karibu yetu, ndiye rafiki mwaminifu, mwenye kututunza na kutukinga. Tumtukuze, tukimheshimu kama mkubwa wetu, tumwamini. Tufuate mashauri yake ili apate kumtolea Mungu sala na matendo yetu kwa furaha.

Maoni
Ingia utoe maoni