Lawrence, Shemasi Na Shahidi
Mtakatifu Lawrence alizaliwa mwaka 225 Desemba 31, huko Valencia, Hispania (wakati huo chini ya utawala wa Warumi ).
Nyakati hizo Mtakatifu Papa Sixtus II, alikuwa mwalimu huko Caesaraugusta (Zaragoza) na alipokwenda Roma, alifuatana na Mtakatifu Lawrence. Na mwaka 257 Mtakatifu Sixtus alipochaguliwa kuwa Papa, alimpa Lawrence daraja la Ushemasi.
Huko Mtakatifu Lawrence akiwa na wenzake 6 walikuwa wakihudumu katika kanisa kuu la Roma.Hivyo aliitwa Shemasi wa Roma.
Mtawala wa Kirumi aliyeitwa Valerian, alipoanza kuwatesa na kuwauwa wakristo mwaka 258 alimkamata na kumuua Papa Sixtus II,mwezi August tarehe 6 ya mwaka huo.
Mtawala huyo, alimwamuru Shemasi Lawrence, kumkabidhi mali zote za kanisa. Shemasi aliomba siku tatu ,kukusanya mali hizo.Akakusanya mali hizo, akawagawia wahitaji na maskini, ili mali hizo zisiingie katika mikono ya watawala.
Siku ya tatu, Shemasi Lawrence alijikabidhi katika mikono ya askari wa mfalme. Alivyoambiwa akabidhi mali alizokusanya, aliwaonyesha kundi la maskini na walemavu kwamba ndio utajiri wa kanisa.
Kutokana na majibu hayo,Shemasi Lawrence alihukumiwa mateso na kifo.Akawekwa katika gereza la San Lorenzo, huko Miranda.
Baadae Shemasi Lawrence aliuwawa kwa kuchomwa katika moto mkali.Ilikuwa mwaka 258 August 10, huko Roma.

Maoni
Ingia utoe maoni