Alhamisi. 03 Aprili. 2025

Mt. Mwenyeheri Yakobo Wa Sale, Padri Na Shahidi

Mwenyeheri Yakobo Wa Sale, Padri Na Shahidi

Mwenyeheri Yakobo wa Sale, alizaliwa mwaka 1556, Marchi 21, Lezoux, Ufaransa. Alisoma katika shule ya wa Jesuit mwaka 1568-1572. Mwaka 1573 alipata ruhusa ya kujiunga na seminari huko Verdun.

Akasoma Filosofia na Teolojia katika chuo kikuu cha Pont-a-Mousson, ambako pia alifundisha. Mwaka 1585 alipata daraja la upadre na akaendelea kufundisha katika chuo kikuu cha Pont-a-Mousson.

Aliomba kwenda kufanya umisionari nje ya Ufaransa, lakini wakuu wake walimwambia kuwa afanye umisionari huo Ufaransa, ambako kulikuwa na mgawanyiko mkubwa kiimani. Hivyo akapewa kazi ya kuweka sawa hali ya mafundisho huko Tournon, ambako kulikuwa na ushindani na uhasama mkubwa uliotokana na mafundisho na mapokeo tofauti.

Akafundisha na kuhubiri sehemu mbalimbali, na mwisho akaenda mji wa Aubenas na akaenda huko akifuatana na Bruda William Saultemouche.

Waliondoka pale wakijua yatakayojili, wakiwaomba wenzao kuwaombea.

Mwaka 1593 Februari 5, Padre Yakobo akifundisha katika moja ya familia, alisikia vishindo na mayowe nje. Akakimbilia kanisani, ili kuokoa Ekaristi takatifu zisichukuliwe na waasi. Huko alimkuta Bruda William, wakaungana na kuhifadhi vitu vyote salama, wakarudi nyumbani kwao.

Kesho yake asubuhi walivamiwa na kukamatwa na askari waasi wa Huguenots, wakahojiwa, wakidhihakiwa na mwisho kuuawa.
Alitangazwa mwenye heri mwaka 1926, Juni 6 na Papa Pius XI.

Maoni


Ingia utoe maoni