Jumatano. 04 Desemba. 2024

Mt. Norbert, Askofu

Norbert, Askofu

Mtakatifu Norbert alizaliwa mwaka 1080, Xanten, Jimbo la Cologne, Ujerumani. Alikua, akasoma vizuri katika mji wa Xanten .

Alichaguliwa kufanya kazi mbalimbali za kanisa na pia kuwa mshauri wa mfalme kuhusiana na dini. Akakataa kupata sakramenti ya upadri. Mwaka 1115, alipanda farasi kwenda mji mwingine, kukatokea tufani kubwa iliyosababisha farasi kumtupa chini.Akakosa fahamu kwa saa nzima,na mwisho akarudi Xanten.

Akakata shauri kujitoa maisha yake kwa Mungu.Akajiweka chini ya Cono, ambaye alikuwa mkuu wa nyumba ya watawa ya Mtakatifu Sigeberg ,karibu na Cologne .Mtakatifu Norbert alipata daraja la upadri akiwa na miaka 35.

Mwaka 1118 alikwenda Roma,ambako alionana na Papa Gelasius II,ambae alimpa ruhusa kuhubiri.Akahubiri Ujerumani,Ubelgiji, Uholanzi na Ufaransa, huku akifanya miujiza mingi.

Mwaka 1119 Papa CalixtusII alimuomba Mtakatifu Norbert kuanzisha shirika, katika jimbo la Laon Ufaransa. Mtakatifu Norbert, aliishi kwa kufuata maisha ya mtakatifu Augustine. Akaanzisha shirika huko Coucy na watu wengi wakajiunga katika muda mfupi.

Wakajenga nyumba zao na kanisa.
Mwaka 1126 Papa Honorius II alichagua mtakatifu Norbert kuwa Askofu wa Magdeburg .Akafanya kazi kwa nguvu na busara,na mwaka 1130 alipochaguliwa Papa Innocent II, Mtakatifu Norbert alimuunga mkono,kwani kulikuwa na kundi lililompinga.

Mtakatifu Norbert alikufa mwaka 1134,na akatangazwa mtakatifu mwaka 1582 na Papa Gregory XIII.

Maoni


Ingia utoe maoni