ALFONSI MARIE DE' LIGUORI, ASKOFU NA MWALIMU WA KANISA
Kanisa linafanya kumbukumbu kwa heshima ya Mtakatifu Alfonsi aliyezaliwa septemba 27, 1696 huko Marienella, Campania,Naples nchini Italia. Akabatizwa siku mbili tu baada ya kuzaliwa kwake na Baba yake alikuwa afisa katika jeshi la wanamaji.
Akasoma katika chuo kikuu cha Naples na kupata Shahada ya Uzamivu katika sheria za nchi na sheria za kanisa.Akawa mwana sheria maarufu.
Akaachana na kazi za sheria na kuamua kumtumikia MUNGU na akapata Daraja la Upadre Desemba 21, 1726. Katika mwaka wake wa kwanza katika Upadre akawa karibu na watu wasio na makazi na maskini.
Mtakatifu Alfonsi akajenga kanisa dogo ambalo lilitumika kwa ajili ya maombi na mahubiri. Alikuwa pia akifundisha watu elimu mbalimbali.Akaanza pia kupata maono kwa mama ,Bikira Maria.
Mnamo November 9, 1732 alianzisha Shirika lililojulikana kama Most Holy Redeemer baada ya kuambiwa na Sista Maria Celeste Crostarosa ambaye alipata maono yaliyomwonyesha jambo hilo.
Mwaka 1762 Mtakatifu Alfonsi alisimikwa kuwa Askofu wa Sant'Aghata dei. Akaandika vitabu na maandiko mbalimbali ya kuwapa moyo watu wanaoamua kujitoa kwa ajili ya Kristo. Akawataka Mapadri kufanya mahubiri na mafundisho yanayotosheleza.
Mwaka 1775 Mtakatifu Alfonsi aliruhusiwa kupumzika na akaenda kuishi huko Pagani Italia ambako alikufa Agosti 1, 1787.
Mtakatifu Alfonsi alitangazwa Mwenyeheri hapo Septemba 1816 na Baba Mtakatifu Pius VII na kutangazwa Mtakatifu Mei 26, 1839 na Baba Mtakatifu Gregory XVI
Maoni
Ingia utoe maoni