Yohani Gualbert
Mtakatifu Yohani Gualbert alizaliwa mwaka 985 huko Florence nchini Italia na alisoma mapema.
Kaka yake wa pekee aliyeitwa Hugo aliuawa.
Mtakatifu Yohani aliamua kuacha vyote ili alipize kisasi kwa kumuua mtu aliyemuua nduguye.
Ikatokea siku ya Ijumaa kuu Yohani aliingia Mjini Florence akifuatana na wenzake,wakiwa na silaha.
Katika njia nyembamba alikutana na muuaji wa kaka yake na akaamua kumuua ili kutimiza kisasi chake.Wenzake wote wakapiga magoti mbele silaha zao wakaziweka kama msalaba wakimuomba Yohani asimuue mtu yule kwa kuwa ilikuwa siku ambayo Wakristu hukumbuka kifo cha Bwana YESU.
Mtakatifu Yohani akamsamehe na akaingia katika Kanisa la Wabenedictine huko San Miniato.
Alipoangalia msalaba uliokuwa mbele yake alitambua kuwa alipaswa kusamehe kwa nia moja na Mtakatifu Yohani Albania akajiunga na Watawa Wabenedictine.
Kwa misimamo ya ukweli wake Mtakatifu Yohani alikosana na mkuu wake na Askofu wa Florence . Aliondoka hapo akaenda Camaldoli na baadaye akaweka makazi yake Vallombrosa.
Huko Mtakatifu Yohani akaanzisha makao mapya ya watawa. Eneo kuzunguka hapo lilikuwa pweke na tupu. Akaanza kupanda miti kulizunguka eneo hilo akishirikiana na watawa wenzie wakatengeneza sehemu nzuri za kusali na mazingira mazuri.
Akawezesha kuanzisha sehemu monasteri zingine akihudumia maskini na wasiojiweza.
Mtakatifu Yohani alikufa mwaka 1073, huko Badia Passignano, Florence katika ardhi ya Taifa la Italia na Baba Mtakatifu Celestine III akamtangaza kuwa Mtakatifu mwaka 1193.
Maoni
Ingia utoe maoni