Mwenyeheri Emmanuel Ruiz na Wenzake, Mashahidi
Mwenyeheri Emmanuel Ruiz alizaliwa Mei 5, 1804 huko Santander katika Taifa la Hispania.
Baada ya masomo yake Mtakatifu Emmanuel alijiunga na Shirika la wa Francisan na akapata Daraja Takatifu la Upadri.
Mwenyeheri Emmanuel Ruiz alienda kufanya kazi huko Damascus nchini Syria akiwa Padri na Mkuu wa Nyumba ya Watawa wa Francisan.
Nyakati hizo kulikuwa na vurugu kubwa iliyosababishwa na waislamu ambao waliwakamata na kuwatesa na kisha kuwaua Wakristo, ambao walishikiria imani yao.
Wauaji walipofika katika Convent ya Wafrancisan Mwenyeheri Emmanuel Ruiz na wenzake 7 pamoja na Walei 3 walikataa kukana imani yao jambo lililopelekea mateso makali na mwisho kuuawa na Ilikuwa mwaka 1860 Mjini Damascus.
Walitangazwa Wenyeheri Oktoba 10, 1926 na Baba Mtakatifu Pius XI
Maoni
Ingia utoe maoni