Jumanne. 03 Desemba. 2024

Mt. Veronika Giuliani

Veronika Giuliani

Kanisa linafanya kumbukumbu kwa heshima ya Mtakatifu Veronika aliyezaliwa Binasco,Milan Nchini Italia mwaka 1660. Alijiunga na Shirika la Watawa Wakapuchini mwaka 1677 huko City de Castello ,Umbria.

Mama yetu Mtakatifu Veronika alibaki huko kwa maisha yake yote kwa miaka 34 na alitumikia nafasi mbalimbali mwisho akawa Mkuu wa Wakufunzi katika Shirika.

Mwaka 1697 Mtakatifu Veronika alianza kupata Stigmata yaani maono ya mateso ya YESU pamoja na madonda yake. Alipata maono mengine mengi sana.

Katika Maisha yake ya unyenyekevu na utii Mtakatifu Veronika aliwavutia sana watawa wenzie kwa uchaji wake. Mwaka 1716 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Convent yao ni nafasi aliyoitumikia mpaka kifo chake.

Mtakatifu Veronika kwa kadri ilivyompendeza MUNGU alimwita kwake mbinguni Julai 9, 1727 na mnamo mwaka 1839 akatangazwa Mtakatifu.

Maoni


Ingia utoe maoni