Jumatatu. 06 Mei. 2024

Mt. Maria Goretti

Maria Goretti

Mama Kanisa anatuomba kuunga naye katika kumbukumbu na heshima kwa Maria Goretti, Mtakatifu aliyezaliwa October 16, 1890 huko Ancona katika ardhi ya nchi ya Italia.

Akiwa na miaka 5 tu Mtakatifu Maria Goretti familia yao ilifilisika hali iliyopelekea kuhama na kufanya vibarua kwa watu mbalimbali.

Waliishi katika nyumba ambayo walichangia na familia nyingine ambapo aliishi Giovanni Serenelli na mwanae aliyeitwa Alessandro . Na akiwa na miaka 8 tu baba yake alikufa.

Julai 5, 1902 Mtakatifu Maria Goretti akiwa na miaka 11 alikuwa nyumbani na mdogo wake Teresa. Mama yake na ndugu zake walikuwa shambani.

Alessandro alirudi nyumbani na kumtishia kumbaka huku akiwa amemshikia kisu Mtakatifu Maria Goretti alimwambia kuwa analotaka kufanya ni dhambi kubwa na akakataa .

Alessandro alimchoma kisu mara 14 na kabla ya kifo chake Maria aliwaambia Madaktari na Polisi tukio lilivyotokea.

Mtakatifu Maria Goretti alikufa Julai 6, 1902 na akatangazwa Mwenyeheri Aprili, 27 1947 na Baba Mtakatifu Pius XII na kutangazwa Mtakatifu mnamo Juni 24, 1950 na Baba Mtakatifu Pius XII.

Maoni


Ingia utoe maoni