Thomas, Mtume
Mama Kanisa anatualika kwenye sherehe ya kumbukumbu kwa heshima ya Mtakatifu Thomas aliyezaliwa huko Galilaya Israeli karne ya kwanza. Aliitwa Thomas maana yake Pacha ( rejea Yohane 11:16) na alikuwa mmoja kati ya Mitume 12 wa Bwana YESU.
Mtakatifu Thomas alikataa habari ya kufufuka kwa Bwana YESU mpaka alipopata uthibitisho wa kugusa majeraha ya Bwana YESU katika viganja na ubavuni pake ( soma Yohane 20:24-29).
Siku ambayo Bwana YESU alipowatokea mitume siku ya nane baada ya kufufuka alimwita Mtakatifu Thomas kugusa majeraha yake ili kumuondolea mashaka. Mtakatifu Thomas alikiri na kusema "Bwana wangu na MUNGU wangu".
Baada ya Bwana kupaa mbinguni Mtakatifu Thomas Mtume alienda kuhubiri katika nchi mbalimbali mpaka India.
Mtakatifu Thomas alikufa huko Parangimalay, Chennai- Tamil Nadu katika ardhi ya Taifa la India mwaka 72 Baada ya Kristo.
Maoni
Ingia utoe maoni