Jumanne. 03 Desemba. 2024

Mt. William wa Vercelli

William wa Vercelli

Kanisa linafanya kumbukumbu ya Mtakatifu William aliyezaliwa mwaka 1085 katika familia bora huko Vercelli nchini Italia.Wazazi walikufa hivyo alilelewa na ndugu.

Mtakatifu William alienda hija katika Mji wa Santiago de Compostela na baadaye akaamua kwenda Jerusalem. Lakini alivamiwa na wezi akaibiwa na kupigwa na akaamua kwenda kukaa Mount Vergine kusini mwa Italia akisali na kuomba.

Hapo alivutia watu wengi Sana ambao waliamua kukaa naye na kufuata mtindo wake wa maisha. Akaanzisha monasteri ya Monte Vergine.

Miujiza mingi ilitendeka jambo lililomfanya Mtakatifu William kuwa maarufu mno na hivyo mwaka 1128 aliamua kuondoka hapo na kwenda kuanzisha makazi mapya huko Geleto karibu na Mji wa Campania.

Kuanzia hapo Mtakatifu William aliweza kufungua nyumba mbalimbali za watawa katika sehemu tofauti.

Mtakatifu William alikufa June 25 , 1142 hapo Geleto na mabaki yake kuhamishiwa Monte Vergine September 2, 1807 kwa amri ya Mfalme Gioacchino wa Naples.

Maoni


Ingia utoe maoni