Jumanne. 03 Desemba. 2024

Mt. Joseph Cafasso

Joseph Cafasso

Mama Kanisa katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa Sita anatualika kufanya kumbukumbu na heshima kwa Mtakatifu Joseph Cafasso aliyezaliwa mwaka 1811 katika mji ulioitwa Castelnuovo d`Asti kwa sasa unajulikana kama Castelnuovo Don Bosco katika mkoa wa Piedmont katika Taifa la Italia. Alikuwa mtoto wa 3 katika familia ya watoto 4 na wazazi wake walikuwa wakulima.

Tangu akiwa mdogo Mtakatifu Joseph aljihisi kuwa anatakiwa kuwa Padri na hivyo alijiunga na Seminari ya Turin kwa masomo. Hapo akakutana na kijana mwingine kutoka mjini kwao aliyeitwa John Bosco.

Mtakatifu Joseph Cafasso alipata Daraja la Takatifu la Upadri Septemba 21, 1833. Alijiendeleza tena na masomo ya Teolojia katika Chuo Kikuu cha Turin ambapo pia alikutana na Luigi Guala mwanzilishi Wa Ecclesiastical College of St Francis of Assis. Chuo kilichosaidia mno mapadri wazawa wa eneo hilo kupata elimu ya juu.

Mtakatifu Joseph alijiunga na chuo hicho kama mwanafunzi na akawa mwalimu na baadaye kuwa Mkuu wa Chuo hicho hapo mwaka 1848. Alikuwa mwalimu mzuri aliyefundisha kwa mifano mbalimbali.

Mtakatifu Joseph Cafasso pia alipata muda mwingi wa kuwaungamisha watu, aliwashauri njia njema za kufika katika malengo yenye baraka na mafanikio. Akatenga muda kwa ajili ya wafungwa katika magereza, akiwahuburi na kuwaungamisha.

Mtakatifu Joseph aliwaliwaza na kuwapa faraja wafungwa waliohukumiwa kifo. Akasaidia wengi kwa ushauri na kuwarejesha katika njia njema.

Mtakatifu Joseph Cafasso alikufa June 1860 akatangazwa Mtakatifu mwaka 1947 na Baba Mtakatifu Pius XII .

Mwaka 1948 Baba Mtakatifu Pius XII alimtangaza kuwa Mwombezi na Msimamizi wa magereza na wafungwa.

Maoni


Ingia utoe maoni