Adalbert
Mama Kanisa anatualika katika kumbukumbu na heshima kwa Mtakatifu Adalbert aliyezaliwa mwaka 910 huko Lorraine ambako sasa ni Taifa la Ufaransa.
Mtakatifu Adalbert alikuwa ni Mtawa katika monasteri ya Mtakatifu Maximinus Tier Ujerumani ambayo ilikuwa ikimilikiwa Watawa wa Wabenedictine.
Mnamo mwaka 961 Mtakatifu Adalbert alipata Daraja Takatifu la Uaskofu na akapelekwa kufanya kazi huko Kiev nchini Urusi.
Mtakatifu Adalbert akiwa nchini Urusi alipata upinzani mkali toka kwa Mwana wa Mfalme na kusababisha kuuawa kwa Wasaidizi wake na hivyo akaamua kuondoka huko akaenda Mainz nchiniUjerumani .
Baadaye akawa tena Askofu wa Magdeburg na huko alifanya kazi nyingi, akaweza kuzindua parokia nyingi.
Mtakatifu Adalbert pia aliwafundisha wanafunzi katika ngazi mbali mbali.
Mtakatifu Adalbert alipokufa June 20, 981 Ujerumani katika Mji wa Zscherben huko Merseberg.
Maoni
Ingia utoe maoni