Jumatatu. 06 Mei. 2024

Mt. Desderius, Askofu na Shahidi

Desderius, Askofu na Shahidi

Mama Kanisa anatualika katika kumbukumbu na heshima kwa Mtakatifu Desderius aliyezaliwa Autun,Gaul huko Ufaransa, alijulikana pia kama Didier.

Baada ya maisha ya utotoni na masomo aliamua kumtumikia Mungu. Akawa Askofu wa Vienne. Kwa jinsi alivyokuwa na msimamo kiimani,alipata maadui wengi mno,akiwemo malkia Brunhildi.Malkia huyo aliamua mpaka kusema uongo kwa papa,kuhusu Askofu Desderius kuwa anajishughulisha na mambo ya wapagani.

Baada ya uchunguzi Baba Mtakatifu Gregory mkuu akamtangaza kuwa Askofu huyo ni safi.

Ila malkia Brunhildi akafanya njama nyingine kumfukuza Askofu huyo hapo Vienne.

Miaka 4 baadaye Askofu Desderius alijaribu kurudi jimboni kwake lakini akauwawa na watumishi wa mfalme Theodoric.

Maoni


Ingia utoe maoni