Jumapili. 05 Mei. 2024

Mt. Augustino wa Canterbury

Augustino wa Canterbury

Kanisa linosafiri linafanya kumbukumbu na heshima kwa ajili ya Mtakatifu Augustino wa Canterbury aliyezaliwa mnamo karne ya 6 nchini Italia.

Alikuwa mkuu wa nyumba ya watawa ya wa Benedictine huko Roma.

Mnamo mwaka 595 Mtakatifu Augustino alichaguliwa na Baba Mtakatifu Gregory Mkuu kuongoza Wamisionari kwenda kuinjilisha huko katika Ufalme wa Kent nchini Uingereza na kumuinjirisha pia mfalme Ethelbert. Kwa kuwa katika wakati huo watawala walikuwa wapagani.

Mwaka 597 Mtakatifu Augustino alifika katika bandari ya kisiwa cha Thanet. Kutokea hapo akaelekea Canterbury kumuona mfalme.

Mfalme Ethelbert alipokea mafundisho, akabatizwa, akaruhusu Wamisionari kuhubiri na kufundisha kwa uhuru.

Aliwapa pia ardhi ya kujenga nje ya kuta za mji. Baadaye Mtakatifu Augustino alichaguliwa kuwa Askofu wa Canterbury.

Kutokana na mafundisho yake alifanikiwa kubatiza watu wengi na katika misa ya Krismasi ya mwaka 597 alibatiza watu zaidi ya elfu moja.

Mwaka 601 Baba Mtakatifu Gregory Mkuu alituma Wamisionari wengine kusaidia kazi pamoja na barua za pongezi na kutia moyo.

Kulikuwa na majaribio kadhaa ya kumpinga yaliyofanywa na wapagani bila mafanikio.

Mtakatifu Augustino alikufa Mei 26, 604 huko Canterbury, Kent huko huko Uingereza.

Maoni


Ingia utoe maoni