Yohane Francesco Regis
Mtakatifu Yohane Francesco Regis alizaliwa Januari 31, 2597 huko Fontcouverte, Aude nchini Ufaransa. Baba yake aliitwa Jean Regis na Mama yake Marguerite de Cugunhan.
Mtakatifu Yohane alianza masomo yake katika Kituo cha wa Jesuit huko Beziers . December 8, 1616 akiwa na miaka 19 aliingia katika shirika la Wa Jesuit huko
Toulouse na akaweka kiapo chake miaka 2 baadaye .
Alipomaliza masomo yake Mtakatifu Yohane alipelekwa kufundisha katika vyuo tofauti. Wakati akifundisha aliendelea pia kusoma Falsafa katika Chuo cha Tournon na 1628 alianza kusoma Teolojia.
Mnamo mwaka 1630 kwa matakwa ya MUNGU Mtakatifu Yohane alipata Daraja Takatifu la Upadri na akapangiwa kufanya kazi katika Chuo cha Montpellier.
Mtakatifu Yohane hapo alifanya kazi kwa bidii, akihubiri, akisaidia wagonjwa na kusaidia wahitaji.
Pia aliweka nguvu kwa Wajane na Yatima, akawafundisha kazi mbalimbali ili kuwawezesha kujitegemea.
Mtakatifu Yohane alikusanya chakula , fedha, nguo na akajenga mabweni kusaidia wasichana makahaba kubadilika.
Mwaka 1633 Mtakatifu Yohane alipata mwaliko kutoka kwa Askofu Louis de la Baume de Suze ambaye alimpa kazi ya kuhubiri katika wilaya 50 tofauti katika Jimbo la Vivarais, Le Feroz na Le Velay.
Kupitia mwaliko huo Mtakatifu Yohane alifanya kazi ngumu kati ya Walei na Mpadri akihubiri na kufundisha.
Mtakatifu Yohane alipomaliza kazi ya utume huko alizunguka pia sehemu nyingi za Ufaransa akifanya kazi ya MUNGU kwa furaha. Sehemu nyingine alipata taabu sana katika usafiri kutokana na mazingira magumu.
Mtakatifu Yohane alipata Ugonjwa wa Nimonia na Desemba 31, 1640 alikufa huko Lalouvesc, Ardeche katika Taifa lake la Ufaransa.
Baba Mtakatifu Clementi XI alimtangaza kuwa Mwenyeheri Mei 18, 1716 na Baba Mtakatifu Clement XII akamtangaza kuwa Mtakatifu Aprili 5, 1737.
Maoni
Ingia utoe maoni