Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Emilia de Vialar

Emilia de Vialar

Mama Kanisa anatualika kumbukumbu na heshima kwa Mtakatifu Emilia de Vialar aliyezaliwa September 12, 1797 huko Gaillac karibu na Toulouse,
kusini mwa Taifa la Ufaransa.

Alizaliwa katika familia ya kikristo na iliyoheshimika sana. Baba yake alikuwa Baron Jacques de Vialar na Mama yake ni Antoinette Portal.

Mtakatifu Emilia akiwa na miaka 7 alianza shule na akaanza kujifunza maisha ya kumcha MUNGU akiwa mdogo.

Mtakatifu Emilia alikataa hata kujitazama katika kioo pale aliponunuliwa nguo mpya.

Akiwa na miaka 13 alipelekwa katika shule ya bweni ambayo ilikuwa katika Convent ya Abbaye- au-Bois huko Paris. Baadaye akarudi Gaillac akiwa na miaka 15. Mama yake alikufa mwaka 1810.

Ndani ya miaka 20 Mtakatifu Emilia alikuwa nyumbani akisaidia mambo mbalimbali. Baadaye akaanza kuwafundisha watoto pamoja na wakubwa waliopoteza imani yao kwa sababu mbalimbali.

Mtakatifu Emilia akajiapia kujitolea maisha yake kwa MUNGU. Mwaka 1832 alipata sehemu ya urithi wake kwa Babu yake.

Akamwacha baba yake akanunua nyumba hapo Gaillac na akaishi na wasichana watatu ambao walikuwa tayari kusaidia katika kuangalia wagonjwa na watoto.

Wakaanza kutunza wahitaji na kutoa misaada kwao.Walisaidiwa pia na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Petro iliyokuwa jirani yao.

Mwaka 1833 wakaanza kufuata sheria za watawa na mwaka huo huo mwezi June tayari kulikuwa na watawa wapatao 26. Miaka 2 baadaye wakaweka nadhiri zao.

Ukawa mwanzo wa shirika jipya la Congregation of the Sisters of Saint Joseph of the Apparition na kazi zao zikiwa kujali watoto,wagonjwa, mahospitali na magereza .

Watawa hao wakaendelea kupata msaada wa Mapadri na Askofu wakiongozwa na Mama Emilia .

Mwaka 1835 Mtakatifu Emilia aliondoka na watawa 3 kwenda Algeria kuanzisha hospitali. Wakafanikiwa na wakapambana na mlipuko wa kipindupindu, huku wakifanya kazi usiku na mchana.

Wakaenda tena katika miji mingine ndani na nje ya Ufaransa wakifungua nyumba za watawa na hospitali. Mwaka 1842 walipata Hati ya Pongezi kutoka Roma kwa Baba Mtakatifu.

Mtakatifu Emilia de Vialar alikufa August 24, 1856 akiacha vituo 42 duniani kote.

Mtakatifu Emilia alitangazwa Mwenyeheri mwaka 1939 na mwaka 1951 akatangazwa Mtakatifu na Baba Mtakatifu Pius XII.

Maoni


Ingia utoe maoni