Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Juliana Falconieri

Juliana Falconieri

Mtakatifu Juliana Falconieri alizaliwa mnamo mwaka 1270 katika familia yenye uwezo kifedha huko Florence nchini Italia.

Baba yake alikufa wakati Juliana akiwa bado mdogo na hivyo alilelewa na mama yake na mjomba wake aliyeitwa Alexis, ambaye naye alishiriki kuanzisha Shirika la Utawa wa Tatu wa Servites.

Akiwa na miaka 15 Mtakatifu Juliana alikataa wazo la ndoa kutoka katika familia yake. Mwaka uliofuatia alijiunga na Wa servite katika ngazi ya tatu. Aliendelea kukaa kwao hadi mwaka 1304 mama yake alipokufa.

Mtakatifu Juliana akajiunga pamoja na kundi la wanawake waliopenda kuishi maisha ya sala na kazi. Wakapanga sheria mpya zilizowapa mwelekeo wao ambazo pia baadaye zilikubaliwa na Baba Mtakatifu Martin V .

Mtakatifu Juliana akawa kiongozi wa kwanza. Katika muda wa uhai wake miujiza mingi ilitokea kutokea kwake.

Alikufa mwaka June 19, 1340. Alitangazwa mwenyeheri Julai 26, 1678 na Baba Mtakatifu Innocent XI na akatangazwa Mtakatifu Juni 16, 1737 na Baba Mtakatifu Clement XII.

Maoni


Ingia utoe maoni