Alhamisi. 21 Novemba. 2024

Mt. Blaise

Blaise

Mt. Blaise alikua ni Askofu wa Sebastia huko Armenia ambaye alifariki kama mfia Dini katika utawala wa Licinius mnamo karne ya nne (4). Mt. Blaise alizaliwa katika familia tajiri lakini yenye maadili iliyomlea kama mkristu toka utotoni. Baada ya kufanywa Askofu, yakaanza mateso makali kwa Wakristu yakifanywa na wapagani. Alipata ujumbe kwa Mungu akaambiwa akimbilie milimani ili kuyakwepa mateso hayo waliyoyapata wakristu. Siku moja wanaume waliokuwa wakiwinda walikuja ligundua pango huko mlimani lililozungukwa na wanyama pori walioshambuliwa na magonjwa mbali mbali. Katikati yao alitembea Mt. Blaise asiyeonekana kujawa na woga akiwazungukia na kuwatibu wanyama hao. Walipogundua kuwa ni Askofu walimkamata ili wakamfungulie mashtaka. Wakiwa njiani, kupitia maajabu yake alifanikiwa kumshawishi Mbwa Mwitu kumwachia nguruwe ambaye alimilikiwa na mwanamke maskini asiye na mali. Mt. Blaise alihukumiwa kifo cha kushindishwa njaa. Wakati yu kifungoni, mwanamke maskini aliyesaidiwa aliweza kupenyeza gerezani na kufanikiwa kumletea mshumaa na chakula. Hatimaye Mt. Blaise alikuja kuuawa na mtawala wa pale kwa kukatwa kichwa.

“Matendo ya Mt. Blaise”
Mt. Blaise ambaye alisoma filosofi katika ujana wake alikua ni Daktari katika mji wa kuzaiwa Sebaste huko Armenia. Alifanya kazi yake ya tiba kwa uwezo wa ajabu wa miujiza, upendo na ucha Mungu. Baada ya Askofu wa mji wake kufariki aliteuliwa kumrithi na hivyo kutambuliwa na watu wote. Ucha Mungu wake ulithibitishwa na miujiza mingi. Kutoka kila kona watu wengi walimfuata kupata tiba za kiroho na kimwili. Hata wanyama walimwijia kupata tiba. Mnamo mwaka 316, Agricola, Gavana Cappadocia na Armenia, baaya ya kufika Sebastia akibeba amri kutoka kwa Mfalme ya kuwakatama na kuwaua wakristu alifanikiwa pia kumkamata Askofu Blaise. Akiwa anapelekwa gerezani, Mama mmoja alimpeleka mwanaye wa pekee miguuni mwa Mt. Blaise. Mwanaye huyu aliyekaribia kufa kwa kukabwa na mfupa wa samaki kwenye koo aliweza kuponywa mara moja. Gavana Agricola baada ya kushindwa kumfanya Mt. Blaise amkane Kristu na Imani yake akaamua kumpiga fimbo na kutoa amri ya kukatwa kichwa. Mt Blaise alikufa kama mfia dini akimshuhudia Kristu

Kumbukumbu ya Mtakatifu Blaise. Wakatoliki wengi waweza kukumbuka siku kuu ya Mt. blaise kutokana na upokeaji wa baraka za uponyaji wa magonjwa mbalimbali lakini haswa magonjwa ya Koo katika Misa inayoadhimisha ukumbusho huo. Mishumaa miwili inayoshikiliwa pamoja inawekwa kwenye koo ya mgonjwa huku Baraka za uponyaji zikitolewa. Tukio hili la ulinzi wa magonjwa ya koo kupitia maombi ya Mt. Blaise yanatokana na matendo ya miujiza ya uponyaji aliyofanya Mtakatifu huyu haswa lile la kumponya mtoto aliyekaribia kupoteza maisha yake kwa kukabwa koo na mfupa wa samaki.

Maoni


Ingia utoe maoni