Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Medardi, Askofu

Medardi, Askofu

Hapo zamani katika Ufaransa ya kaskazini palikuwa na mwanamke mkristu aliyetaka kuweka nadhiri ya ubikira, jina lake Protagia. Lakini alibadili nia yake, akaolewa na mkatekumeni jina lake Nektari. Walifunga ndoa, wakapata mtoto aliyeitwa Medardi. Medardi huyu alikuwa mkristu wa kawaida kwa muda, lakini alipokuwa na umri wa miaka thelathini na mitatu alipewa upadre. Hatujui mambo mengi juu ya maisha yake, ila alipokuwa mzee, alichaguliwa kuwa Askofu wa Tournee (Tournay, Ufaransa). Ijapokuwa alikuwa mzee, nguvu yake na bidii yake zilikuwa kama za mtu wa makamo tu.

Habari za kale zinasema kwamba Mtakatifu Medardi alizoea kutoa mfuko wa fedha na taji la mawaridi kila mwaka kwa kijana mwanamke aliyewapita wenzake kwa tabia na mwenendo bora. Desturi hii iliendelea miaka mingi sana huko jimboni mwa Swasoni (Soisson, Ufaransa). Katika sikukuu ya Mtakatifu Medardi, baada ya Baraka msichana aliyekubaliwa na watu wa kijiji kwamba aliwapita wenzake kwa mwenendo wake bora, alivikwa nguo nyeupe. Baadaye padre alimvika taji la mawaridi kichwani na kumpa tuzo lake. Yasemekana kuwa huko wanawake husifiwa kwa mienendo yao bora na adabu njema.

Maoni


Ingia utoe maoni