Marselino na Petro
Habari za kifo cha wafiadini hawa waliokufa wakati wa madhulumu ya wakristu yaliyofanywa na Kaisari Dioklesiani, ziliandikwa na Papa Damasi, ambaye yeye naye alizipata kwa yule aliyehusika na kifo chao. Wafiadini hawa Marselino na Petro wanatajwa katika sala ya Ekaristi ya Kwanza ya Misa pamoja na wafiadini wengine.
Marselino alikuwa padre mjini Roma (Italia), Petro alikuwa mwinga mashetani. Katika masimulizi mengine, inasemekana kwamba Marselino na Petro walitupwa gerezani, na huko waliwaimarisha wakristu katika imani, na pia waliwaongoa wengi. Walipelekwa mahali pa faragha, wakakatwa vichwa.
Amani ilipoenea katika utawala wa Roma, lilijengwa kanisa kubwa juu ya kaburi lao kwa amri ya Kaisari Konstantino, na katika kanisa hilo alizikwa pia Mtakatifu Helena, mama yake Konstantino
Maoni
Ingia utoe maoni