Paulo Miki na Wenzake
Mtakatifu Paulo Miki mwenye asili ya Japan alikua Mkatoliki wa Shirika la Jesuit. Alifariki kama mfia dini (Februri 5, 1597) akiwa kati ya wale wafia dini 26 wa nchi ya Japan ambao Kanisa pia limewatambua kama Watakatifu. Hii ilitokea katika mji uliofahamika haswa kwa kuwa na idadi kubwa sana ya ukatoliki kutokana na jitihada za M-Jesuit Mtakatifu Francis Xavier.
Mt. Paul Miki alizaliwa kwenye familia yenye utajiri mkubwa. Alipata elimu yake kupitia shirika la Jesuit huko Azuchi na Takatsuki nchini Japan. Rasmi alijiunga na shirika hilo la Jesuit na kufahamika na wengi kama mhubiri mashuhuri aliyefanikiwa kuwaleta wengi katika imani ya Kristo ya Kanisa Katoliki. kutokana na hofu ya kuenea kwa kasi imani ya katoliki nchini Japan, Watawala wa Japan walifanikiwa kuwafunga Mt. Miki pamoja na wenzake. Yeye pamoja na wenzake wakatoliki waliamuriwa kutembea maili 600 sawa na kilomita 966 kutoka Kyoto mpaka Nagasaki. Kutokana na Imani yao kubwa waliimba mwimbo wa kumtukuza Mungu njia nzima. Walipofika Nagasaki (Mji wenye Idadi kubwa ya Wakatoliki nchini Japan), Mtakatifu Miki alisulubiwa msalabani kama Kristu mwaka 1597 February. Akiwa msalabani akatoa mahubiri yake ya mwisho akisisitiza kuwa amewasamehe waliomsulubu na kusisitiza kuwa yeye ni MJapan. Yeye alisulibiwa pamoja na wenzake 26 na mnamo mwaka 1862, Baba Mtakatifu Papa Pius IX aliwatambua kama Watakatifu
Akihubiri wakati yuko msalabani alisema:
“Hukumu kwangu na wenzangu inasema sisi tumekuja Japan kutoka nchini Filipino, lakini sikutokea nchi nyingine bali mimi ni mjapani kamili. Sababu moja tu ya mimi kusulubiwa ni kwamba nimefundisha Injili ya Kristo. Ni kweli nimefundisha Injili hiyo. Ninamshukuru Mungu ninakufa kwa jambo hilo. Naamini kwamba nimefundisha ukweli kabla ya mauti yangu. Ninafahamu mnaniamini lakini pia nataka niwaambie mara nyingine, ninamuomba Kristu awasaidie muwe na furaha. Nina mtii Kristu na kwa mfano wake ninawasamehe walioniua. Siwachukii bali namuomba Mungu awasamehe na ninatumai damu yangu itawaangukia wakristu wenzangu kama mvua yenye faida”
Maoni
Ingia utoe maoni