Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Walburga

Walburga

Walburga alizaliwa Uingereza, alikuwa dada wa Watakatifu Wilibaldi na Winebaldi ambao wote wawili walifuatana na Mt. Bonifasi kwenda Ujerumani kama Wamisionari.

Baada ya kujiunga na Utawa, Walburga aliombwa kwenda Ujerumani pamoja na baadhi ya wenzake, na kufungua nyumba ya utawa kule. Kabla ya kuondoka sista Walburga alisomea uganga apate kuwasaidia wagonjwa Kimwili pia. Kule Ujerumani akawa mama Mkuu wa Jumuiya yake ya watawa, na wakati ule ule ndugu yake Winebaldi alikuwa Abati wa watawa wanaume. Ajabu ni kuwa baada ya kifo cha Winebaldi, Askofu wa jimbo alimwomba Sista Walbruda ashike wadhifu wa ndugu yake. Hivyo sista Walbruda aliyekuwa Mkuu wa nyumba ya masista, akawa pia Mkuu wa monasteri ya watawa wanaume.

Alifariki mnamo mwaka 779, miaka mitatu tuu baada ya kifo cha ndugu yake Mt. Winebaldi, akazikwa upande wake katika kanisa la Parokia mjini Eichstat (Ujerumani). Habari yake nzuri imeenea sana kwa sababu ya aina ya mafuta yenye nguvu ya pekee ambayo hutiririka kupitia tundu katika mwamba ambao juu yake masalia yake yamewekwa. Husemwa kwamba kwa nguvu ya mafuta hayo, wagonjwa wamepata kuponywa, hata siku hizi.

Maoni


Ingia utoe maoni