Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Zenobi

Zenobi

Mtakatifu Zenobi alikuwa Padre wa jimbo la Sidoni (Lebanoni). Alijulikana kwa ujuzi wake wa dawa, hivyo alikuwa pia mganga. Siku zake za utume zilikuwa siku zilezile za udhulumu wa Wakristu. Katika mwaka 304, wakristu wengi waliteswa ili waikane dini yao, na kuabudu mungu wa uwongo. Kishawishi kikubwa wakati huo kilikuwa kukana dini. Padre Zenobi alijulikana sana kwa mashauri yake ya kuhimiza Wakristu wabaki katika Imani. Yeye pamoja na Askofu wake Tirannio anayeheshimiwa pia kama Mtakatifu, walijitahidi sana.

Mwandishi mmoja wa historia, jina lake Eusebio, alikuwepo akishuhudia mateso hayo na aliandika jinsi wakristu walivyokufa kama mashahidi shujaa. Wakristu Waafrika kutoka Misri na sehemu nyingine waliteswa kwa kupigwa, kuchomwa moto na hata kutupwa kwenye zizi la wanyama wakali. Lakini Mungu aliwalinda Wakristu hawa, akizuia wanyama wale wakali wasiwadhuru kinyume cha watesi wao. Wanyama hao waliwakimbiza wale waliokuwa watesi wa Wakristu. Baada ya kuwatesa Wakristu kwa namna nyingi, amri ilitolewa wakatwe vichwa, wengine walichomwa moto. Wafiadini walioungama dini yao nyakati hizo waliweza kufanya hivyo kwa kutiwa moyo na Mtakatifu Zenobi.

Miaka sita baada ya udhalimu huu, Zenobi na Askofu wake Tirannio walitiwa nguvuni wakati wa enzi ya Kaisari Maksimini. Wote wawili waliteswa sana, na mwishowe waliuawa mwaka 310.

Maoni


Ingia utoe maoni