Alhamisi. 21 Novemba. 2024

Mt. Josephine Bakhita

Josephine Bakhita

Mt. Bakhita Josephine alizaliwa mwaka 1869, katika kijiji kidogo katika eneo la Darfur nchini Sudan. Yeye alitekwa nyara wakati akifanya kazi katika mashamba na familia yake na hatimaye kuuzwa utumwani. Watekaji wake walimuuliza jina lake lakini kwa kuwa alijawa na hofu kubwa alishindwa kukumbuka. Hivyo watekaji wakamuita "Bakhita," ambayo ina maana ya "bahati" kwa Kiarabu.
Mt. Bakhita alikuja jaliwa bahati sana, lakini miaka ya kwanza ya maisha yake haikushuhudia hilo. Kama mtumwa alipata mateso makali sana na wamiliki wake mbali mbali ambao walimtupia majina, wakampiga na kumkata. Katika wasifu wake anabainisha teso moja la kutisha wakati ambapo mmoja wa wamiliki wake alimkata mara 114 na akamwaga chumvi katika majeraha yake ili kuhakikisha kwamba makovu yanabaki. "Nilihisi Mimi ningelienda kufa wakati wowote, hasa wakati wakisugua majeraha yangu na chumvi," Bakhita aliandika.

Alivumilia mateso yake kwa ushujaa ingawa hakumjua Kristo au asili ya ukombozi na neema katika mateso. Mt. Bakhita pia na mshangao fulani kwa maumbile ya dunia na muumba wake. "Ukiangalia jua, mwezi na nyota, nikajisemea: 'Nani anaweza kuwa Bwana wa mambo haya mazuri?' Na nilihisi hamu kubwa ya kumwona,kumjua yeye na kumtolea heshima. "

Baada ya kuwa ameuzwa jumla ya mara tano, Bakhita alinunuliwa na Callisto Legnani, Balozi Italia huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan. Miaka miwili baadaye, mmiliki huyo alimchukua Bakhita huko Italia ili afanye kazi ya kulea watoto kwa rafiki yake Augusto Michieli. Yeye Augusto, kwa upande wake, alimtuma Bakhita kuongozana na binti yake shule huko Venice. Shule hiyo ilimilikiwa na Masista watawa wa Canossian.

Mt. Bakhita alijihisi amepewa wito wa kujifunza zaidi kuhusu Kanisa, akabatizwa na jina la "Josephine Margaret." Wakati huo huo, Augusto Michieli alitaka kumchukua Mt. Josephine (Bakhita) na binti yake ili awarudishe Sudan, lakini Mt. Josephine alikataa kurejea.

Kutokana na hali hiyo ya kupingana na kutokubaliana Mt. Bakhita alipelekwa mahakamani Italia ambapo Mahakama iliamuru kwamba Mt. Josephine Bakhita anaweza kubaki nchini Italia kwa sababu yeye alikuwa mwanamke huru. Hali ya Utumwa haikutambuliwa nchini Italia na alikuwa pia ni kinyume cha sheria nchini Sudan tangu kabla Mt. Josephine hajazaliwa.

Mt. Josephine alibakia nchini Italia na aliamua kujiunga na Masista watawa wa Canossians mwaka 1893. Alipata taaluma yake mwaka 1896 na alitumwa huko Italia ya Kaskazini, ambapo alijitolea maisha yake kusaidia jamii yake na kuwafundisha wengine kumpenda Mungu.

Alijulikana kwa tabasamu, upole wake, na utakatifu wake. Aliwahi kunukuliwa akisema, "Kama ningebahatika kukutana na wafanyabiashara wa utumwa walioniteka nyara na kunipa mateso makali, ningewapigia magoti na kubusu mikono yao, kwa maana kama kwamba isingalitokea hivyo, nisingalikuwa Mkristo na mwenye dini leo. "

Mt. Josephine alifanywa mwenye heri mwaka 1992 na utakatifu ukafuata muda mfupi baada ya Oktoba 2000 baada ya kutambuliwa na Baba Mtakatifu Yohane Paulo II. Yeye ni mtu wa kwanza kutambulika kama Mtakatifu na anafahamika kama Mtakatifu mlinzi wa nchi ya Sudan.

Maoni


Ingia utoe maoni