Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Silvini

Silvini

Mt. Silvini alitumwa na Baba Mtakatifu kwenda kuhubiri Habari Njema popote aendapo, ndiyo maana hakuwa na kikao kimoja; lakini hata hivyo, alifundisha zaidi watu wa Ufaransa ya Kaskazini. Alifurahi kuona jumuiya ya watu imeongoka. Wakristu wote walimheshimu kama mtu wa Mungu. Ukarimu wake ulisifiwa pote.

Alitumia Mali yake mwenyewe kuwakomboa watumwa. Mali yake nyingine aliitumia kwa kuwasaidia wenye shida na kujenga makanisa. Watu waliona kwamba yeye aliwapokea katika nyumba yake isiyo na fahari kila mgeni aliyefika kana kwamba angekuwa Kristu mwenyewe. Mwandishi wa historia ya maisha yake anasema kwamba kwa muda wa miaka arobaini Mt. Silvini hakula mkate bali aliishi kwa kula majani na matunda.

Maoni


Ingia utoe maoni