Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Katarina wa Risi

Katarina wa Risi

Katarina alizawa Risi (Italia) mwaka 1519 na alipokuwa na umri wa miaka kumi na mitatu aliingia katika Shirika la Mt. Dominiko. Baada ya muda, akawa Mama Mkuu wa Shirika hilo. Kwa upole na uvumilivu wake, alikuza fadhila zake kwa moyo mkubwa kwa kufanya kitubio.

Katarina alijishugulisha sana kuleta mabadiliko katika Kanisa. Hii inajulikana kutokana na barua zake nyingi, ambazo aliwaandikia watu wa ngazi za juu. Alikuwa na uhusiano na wapenda-mapinduzi wa nyakati hizo kama vile Mt. Filipo Neri , Mt. Karoli Boromeo na Mt. Pius wa Tano .

Aliandika barua nyingi na Mt. Filipo Neri, na ijapokuwa walijawa hawakupata kukutana, yeye, Mt. Katarina alimtokea na kuzungumza naye Roma bila kuondoka katika Konventi yake ya Prato. Jambo hili lilisemwa wazi na Mt. Filipo Neri ambaye alikuwa mtu mwangalifu sana kusadiki au kutangaza mambo juu ya watu kutokewa. Jambo hili la kutokewa yeye na Mt. Katarina lilithibitishwa kwa viapo na mashahidi watano.

Mt. Katarina aliitwa Mbinguni na Mchumba wake Yesu mwaka 1589. Alitangazwa kuwa Mtakatifu Mwaka 1746.

Maoni


Ingia utoe maoni