Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Katarina wa Sweden

Katarina wa Sweden

Katarina Ulfedotter alikuwa mtoto wa nne kati ya watoto wanne wa Mt. Birgita, mjane na mtawa. Alipokuwa bado mdogo alikabidhiwa kwa masista wamlee katika konventi yao.

Katarina aliposeshwa na wazazi wake kwa mtu mmoja maarufu na mcha Mungu, ndoa ikafungwa kwa Ibada na sherehe. Lakini katarina anasifika kwa ubikira wake, maana husemwa kwamba yeye na mumewe tangu mwanzo waishi maisha yao yote bila kutumia ndoa yao. Hata hivyo Katarina alimpenda sana mumewe.

Baba wa Katarina alipokwisha kufa, Mama yake Birgita alienda kuishi Roma (Italia). Kwa ruhusa ya mumewe Katarina alikwenda kumtembelea mama yake huko Roma. Alipokuwa huko, mumewe akafariki. Yeye pamoja na mama yake walikwenda kuhiji Asizi (Mt. Fransisko) na nchi takatifu. Licha ya sala alizozoea kusali tangu utoto wake, Katarina akawa sasa anakaa saa nne akiyatafakari mateso ya Yesu. Hawakumsikia hata mara moja akisema maneno ya hasira au dharau kwa wengine.

Mama yake alipokwisha kufa, Katarina akarudi Sweeden ambako alifariki dunia tarehe 23 Machi, 1351.

Maoni


Ingia utoe maoni