Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Oswaldi

Oswaldi

Mtakatifu Oswaldi alizaliwa Uingereza, lakini wazazi wake walitoka nchi ya Denmark. Alikaa kwa mjomba wake Mt. Odo, Askofu Mkuu wa Kanterburi. Kwa uongozi wake ilimbidi kwenda Ufaransa kusomea kanuni za watawa wa Mt. Benedikto. Aliporudi katika nchi yake, aliwekwa kuwa askofu wa Worcester, halafu pia alikuwa Askofu Mkuu wa York. Askofu Oswaldi alipitisha sheria ya kuwataka mapadre wa jimbo waishi maisha ya useja, akatamani kuwarudisha katika Utakatifu wao wa awali.

Askofu Oswaldi alizoea kila siku kuwaosha miguu maskini kumi na wawili, kisha akawakaribisha mezani kwake kwa chakula. Tarehe 29 Februari, mwaka 992, alipomaliza kupangusa na kubusu miguu ya maskini wa mwisho, huku amepiga magoti na kusema: "Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu", akaiaga dunia kwa utulivu wote.

Maoni


Ingia utoe maoni