Agata
Agata alikuwa msichana wa jamaa bora, nzuri na tajiri. Basi, Kwinsiano, Gavana wa Sisilia, alitamani sana kumwoa kwa sababu ya uzuri wake. Agata alikataa kishujaa akisema kwamba amekwisha olewa na mchumba mwingine, yaani Yesu Kristu Mwana wa Mungu mwenyewe. Kwinsiano kusikia hivyo alikasirika sana. Basi, aliamuru watesi wamtese vikali. Wakayakata matiti ya Agata kwa nguvu, na kumlaza mzima juu ya makaa ya moto. Nchi ilitetemeka. Kwinsiano alikimbia maana watu walimkasirikia wakisema kuwa Mungu anaiadhibu nchi kwa sababu ya Ubaya wake. Agata alirudishwa gerezani na mara alizimia roho.
Mwaka mmoja baada ya hayo mlima Etna ulitoa moto, nchi yote karibu ingeteketea. Lakini watu wa Etna walimkimbilia Mwenye heri kwenye Kaburi la Agata, walitwaa shela, wakaielekeza upande wa mlima uliokuwa ukitokota moto. Mara moto ulizimika, na watu wa Etna waliokoka. Ndiyo sababu Mt. Agata huheshimiwa sana katika Italia yote.
Maoni
Ingia utoe maoni