Jumamosi. 18 Mei. 2024

Mt. Ansgari

Ansgari

Ansgari alizaliwa huko Ufaransa mwanzoni mwa karne ya tisa, labda mwaka 801. Alielimishwa katika monasteri. Mnamo mwaka 826 alianza kuhubiri Injili katika ya Denmark. Huko Denmark hakufanikiwa sana, akaenda Sweden. Baadaye, aliteuliwa na Papa kuwa Askofu wa Hamburg (Ujerumani). Papa alimfanya pia kuwa mjumbe wake katika nchi za Denmark na Sweden. Alikabiliwa na matatizo mengi sana katika kazi yake ya kueneza Injili, lakini hakukata tamaa.

Askofu Ansgari alikuwa mhubiri hodari sana, na aliwasaidia watu fukara kwa namna ya pekee: aliwaosha miguu yao na kuwapelekea chakula yeye mwenyewe. Siku moja aliposikia mtu fulani akimsifia kwa miujiza yake, Ansgari alimkaripia hivi: "Mungu angaliniambia unaweza kuomba mwujiza unaopenda, ningalimwomba muujiza mmoja tu: atumie nguvu yake niwe mtu mwema".

Mtakatifu Ansgari alikuwa wa kwanza kupeleka habari Njema ya Injili huko Sweeden. Kisha kufa kwake lakini (mwaka 865), watu waliacha dini ya Kikristu wakawa tena wapagani. Dini ya Kikristu ilirudi tena wakati wa Mt. Sigfridi baada ya karne mbili.

Maoni


Ingia utoe maoni