Jumamosi. 18 Mei. 2024

Mt. Blasi, Askofu na Mfiadini

Blasi, Askofu na Mfiadini

Hata siku hizi Wakristu huzoea kumwomba Mtatifu Blasi msaada katika maradhi na magonjwa ya koo, kwa sababu Mtakatifu huyu alimponyesha mtoto mmoja aliyenusurika kufa kwa miiba ya samaki iliyomkwama kooni.

Blasi alikiwa Askofu wa Sebaste katika Armenia (Uturuki). Inasemekana ya kwamba wakati wa dhuluma Askofu Blasi alikwenda kukaa katika pango porini. Lile pori lilikuwa na wanyama wa mwitu wa kila aina. Blasi aliwatunza wanyama walipokuwa na ugonjwa au jeraha. Siku moja wawindaji wapagani walimkuta katikati ya wanyama hawa. Walishangaa sana, lakini walimpeleka kwa Liwali Agrikola. Liwali huyu aliamuru ateswe mpaka akane dini ya Kikristu. Blasi alikuwa imara katika Imani na mwishowe alikufa shahidi wa dini, walipomkata kichwa chake.

Maoni


Ingia utoe maoni