Jumamosi. 18 Mei. 2024

Mt. Gilidas Mwenye Hekima, Abati

Gilidas Mwenye Hekima, Abati

Mt. Gilidas alizaliwa Uingereza mnamo mwaka 500, akawa baadaye Padre, alafu akawa monasteri. Alikuwa mtu aliyeelimika sana na alijua sana Biblia, ndiyo maana anaitwa 'Mwenye Hekima.

Anasifika kwa ajili ya kitabu alichoandika, ambamo anawalaumu vibaya Wafalme wa nyakati zake pamoja na watu na mapadre wao. Mt. Gilidas alikuwa ameng'amua kuwa jambo baya kuliko yote kwa binadamu ni dhambi. Aliishi miaka yake ya mwisho katika kisiwa kidogo kama mtawa, akiwa na wafuasi kadhaa pamoja naye. Alikufa mwaka 570.

Maoni


Ingia utoe maoni