Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Timoteo, Askofu

Timoteo, Askofu

Baba wa Mtakatifu Timoteo alikuwa mpagani, na mama yake alikuwa Myahudi. Timoteo aliongoka akawa Mkristu wakati Mt. Petro alipomkuta katika Listra, mji wake alimozaliwa (Uturuki). Aliongozwa na Mtume huyu mkuu. Timoteo hakukawia kuendelea katika fadhila zote, hata Mt. Paulo anasema kwamba alikuwa mwanafunzi wake mpenzi.

Timoteo alimsaidia Mt. Paulo kueneza dini ya kweli katika miji ya Ugiriki na Asia Ndogo (Uturuki na Siria) Alipewa daraja ya Uaskofu na Mt. Paulo ili awaongoze Wakristu wasiokuwa Wayahudi. Alitawala kwa sifa jimbo lake la Efeso (Uturuki). Katika mji wa Efeso, palikuwa na hekalu la Diana, Mungu wa uongo. Kila mwaka wapagani walizoea kutolea sadaka na kufanya michezo mibaya mbele ya sanamu hiyo. Siku moja wapagani walizitembeza sanamu za uongo wakicheza ngoma mbaya, na kuimba nyimbo zisizofaa. Hapo Timotea alishikwa na hasira kubwa hivi kwamba alitoka nyumbani kwake, akawakaripia wapagani waliokuwa kama wenda wazima. Walikasirika sana kusikia makaripio na matukano yake. Basi, walimrukia Timoteo wakamponda na kumpiga magongo mwili mzima. Walipokwisha kumuua walibururaburura maiti yake mpaka hasira yao ikatulia.

Maoni


Ingia utoe maoni