Jumamosi. 04 Mei. 2024

Mt. Yohane Paulo wa Pili

Yohane Paulo wa Pili

Mtakatifu YOHANE PAULO II, PAPA. Alizaliwa huko Polandi Mei 18, 1920 na jina lake halisi la ubatizo ni Karol Wojtyla. Kama ilivyo kwa makuhani wa MUNGU naye alipitia masomo katika seminari mbalimbali na hatimaye akapadilishwa Novemba 1, 1946.

Alikuwa Paroko katika Jimbo Kuu la Krakow katika nchi yake Polandi kuanzia mwaka 1948 hadi 1951.

Mnamo Julai 4, 1958 Papa Pius XII alimteua kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Krakow na pia aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo na Papa Paulo VI hapo tarehe 30/12/1963.

Nyota njema huonekana tangia asubuhi mnamo Februari 26, 1967 aliteuliwa kuwa Kardinali na Baba Mtakatifu Paulo VI.

Mapenzi ya MUNGU yalitimia hapo Oktoba 16, 1978 ambapo alichaguliwa kuwa Kiongozi wa Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume au BABA MTAKATIFU au PAPA kama wengi tulivyozoea kuita. Alikuwa Papa wa kwanza ambaye si mtaliano kwa muda mrefu tangia Papa Adrian VI.

kipindi chake cha uongozi wake alikuwa kweli Mtume halisi wa karne na aliweka historia ya kuwa Papa wa kwanza kufanya Hija za Kitume ( ziara) kuliko Papa yeyote na alitembea karibu pembe zote za dunia na ni Papa wa kwanza kufika Tanzania tangia mwanzo wa kuumbwa ulimwengu hapo Septemba 1-5, 1990.

MUNGU alimwita kwa utulivu mkubwa katika ufalme wake hapo tarehe 2/4/2005.

Papa Benedict XVI alimtangaza Mwenyeheri Mei 1, 2011 na kutangazwa rasmi kuwa Mtakatifu Aprili 27, 2014 na Baba Mtakatifu Fransisco.

Maoni


Ingia utoe maoni