Jumapili. 19 Mei. 2024

Mt. Yohani Mtoa Sadaka, Askofu

Yohani Mtoa Sadaka, Askofu

Mt. Yohani alikuwa mtu wa familia ya Kisharifu. Baada ya kufiwa na Mkewe na wanae huko Ziwani Kupro, alitumia mali yake kuwasaidia maskini. Alipokuwa na umri wa miaka karibu hamsini, aliteuliwa kuwa Patriarka (Askofu Mkuu) wa Aleksandria (Misri) akiwa bado Mkristo Mlei.

Alipofika tu Aleksandria Mt. Yohani aliamuru iandikwe orodha kamili ya "Mabwana" wake. Alipoulizwa hao ni akina nani, alieleza kuwa anataka kusema watu maskini, maana hao wana uwezo mkubwa Mbinguni wa kuwasaidia wale ambao waliwatendea mema hapa duniani. Idadi yao ilikuwa 7,500 naye akawa mlinzi wao. Alitoa matangazo ya kuwaamuru watu wote watumie mizani na vipimo vilivyo sawa, ili kuwaepusha maskini wasinyonywe. Aliwataka kabisa maofisa na watumishi wake wote wasipokee zawadi, maana aliona zawadi hizi ni kama rushwa.

Jambo la kwanza alilofanya alipofika Aleksandria ni kugawanya vipande elfu nane vya dhahabu alivyovikuta katika sanduku la hazina la kanisana lake. Alivigawa kwa hospitali na monasteri mbali mbali. Alijenga na kuzipa ruzuku hospitali, kliniki, nyumba za wazee na watu wasiojiweza, hata nyumba za kulala wasafiri. Yeye mwenyewe patriakra aliishi maisha magumu ya Ufukara.

Alipoona kwamba watu wengi wanaoenda kuzungumza nje ya kanisa wakati wa Ibada, Mt. Yohani alienda akakaa kati yao na kusema: "Wanangu, mchungaji ni lazima awe pamoja na kundi lake". Waliona haya kwa kejeli hiyo, hata hawakurudia tena dharau walilozoea kulifanya.

Katika waosia wake aliandika kwamba alikuta sanduku la hazina ya kanisa yake limejaa, lakini aliliacha tupu: "Nimejitahidi kumpa Mungu mambo ambayo ni ya Mungu". Alikufa mwaka 619 au 620.

Maoni


Ingia utoe maoni