Jumapili. 24 Novemba. 2024

Mt. Sebastiano, Mfiadini

Sebastiano, Mfiadini

Sebastiano alikuwa askari aliyewasaidia Wakristu waliokuwa wanateswa na kufukuzwa siku zile. Alishikwa na kupelekwa kwenye baraza la Kaisari Dioklesiano, akashtakiwa kwamba alikuwa mfuasi wa Yesu Kristu. Kaisari alimhukumu auawe kwa kupigwa Mishale. Askari waliompiga mishale walidhani amekwishakufa, basi, wakamwacha pale pale.

Alikuja mjane Mtakatifu jina lake Irena ili amzike, lakini alipomwona anavuta pumzi alimchukua kwake akamtunza kama mwanawe. Sebastiano alipona. Bila hofu alimwendea Kaisari aliyekuwa akienda kwenye hekalu la miungu ya uwongo, akamgombeza akimwambia anawatesa bure Wakristu walio raia zake waaminifu. Kwanza Dioklesiano alishikwa na hofu alipomwona mtu aliyeaminiwa kwamba alikuwa amekwisha kufa. Alitoa amri apigwe magongo mpaka afe, kisha mwili wake ufichwe Wakristu wasije mchukua tena. Lakini mwanamke Mkristu aligundua masalia yake, akayazika kwa heshima karibu na Njia Appia

Maoni


Ingia utoe maoni